Lyrics

Usifurahi juu yangu eh adui yangu
Niangukapo mimi nitasimama tena
Kumbuka niwapo gizani bwana ni nuru yangu
Hawezi kuniacha bwana mimi niangamie
Usifurahi juu yangu eh adui yangu
Niangukapo mimi nitasimama tena
Kumbuka niwapo gizani bwana ni nuru yangu
Hawezi kuniacha bwana mimi niangamie

Si vyema kunisema vibaya nipatapo tatizo
Shetani wampa nafasi katika moyo wako
Kumbuka kwa maombi yako, nitasimama tena
Na utapata baraka kutoka kwake Mungu
Si vyema kunisemasema vibaya nipatapo tatizo baba
Shetani wampa nafasi ndani moyo wako
Kumbuka kwa maombi yako, nitasimama tena
Na utapata baraka kutoka kwake mungu

Lyrics continue below...

Don't want to see ads? Upgrade Now

Maana heri mtu yule ambaye kinywa chake
Huwabariki wenzake na kuwaombea
Maana maneno mabaya huchafua moyo
Ukuwe kama nina Mungu, ni vyema uwe safi

Ukiona nipo kwenye shida niombee
Ndoa yangu imevunjika wewe niombee
Nikifukuzwa kazini ndugu niombee
Magonjwa yananiandama niombee
Biashara haina faida niombee
Nikikawia kupata mtoto niombee
Nimekuwa mtoto yatima niombee
Hata nijapokuwa mjane niombee

Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa
Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa

Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa
Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa

Writer(s): Upendo Nkone

Don't want to see ads? Upgrade Now

API Calls

Scrobble from Spotify?

Connect your Spotify account to your Last.fm account and scrobble everything you listen to, from any Spotify app on any device or platform.

Connect to Spotify

Dismiss